RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ERIC SHIGONGO, MASANJA MKANDAMIZAJI WANOGESHA 'SUNDAY CELEBRATION SEASON 4' YA GWT




Eric Shigongo akitoa somo la Siri za kutoka kuwa Mwajiriwa hadi kuwa Mwajiri kwa watu waliohudhuria Sunday Celebration ya GWT.



Emmanuel Mgaya 'Masanja Mkandamizaji' akitoa burudani kwa wahudhuriaji wa Sunday Celebration.

Shigongo akicheza na baadhi ya wahudhuriaji.

MJASIRIAMALI na Mtunzi Mahiri wa Vitabu Afrika, Eric Shigongo jana Jumapili alitoa somo lake la Siri za kutoka kuwa Mwajiriwa hadi kuwa Mwajiri katika mwendelezo wa programu ya kikundi cha kumsifu na kumwabudu Mungu cha Glorious Worship Team (GWT) ya Sunday Celebration ambayo hufanyika kila Jumapili kuanzia saa 9 alasiri baada ya ibada kwenye Ukumbi wa Victoria Petrol Station, Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Mbali na Shigongo, pia komediani maarufu nchini ambaye pia ni mwimbaji wa nyimbo za Injili, Emmanuel Mgaya 'Masanja Mkandamizaji' naye alikuwepo kuipamba siku hiyo kwa nyimbo za injili.

Waimbaji wengine waliotoa burudani katika siku hiyo ni pamoja na Upendo Nkone, Carvary Band, The Jordan Moses Zamangwa (Mosax).

Akizungumza na tovuti hii, Mkurugenzi wa GWT, Emmanuel Mabisa amesema wiki hii katika Sunday Celebration Season 5, Eric Shigongo ataendelea kutoa somo lake la Siri za kutoka kuwa Mwajiriwa hadi kuwa Mwajiri na katika somo hilo atatoa bure vitabu vyake zaidi ya 200 alivyoahidi kuvitoa kwa watu waliowahi kufika ukumbini katika Sikukuu ya Pasaka.

Comments