RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KANISA LA EFATHA MWENGE: UNAPOBEBA UTAKATIFU UNAKUWA TISHIO KWA KILA KITU KINACHOKUTISHIA NA UNAKUWA TISHIO KWA WANAOKUTISHIA

Kwa msaada wa Mungu, Rumafrica iliweza kuhudhuria Ibada Takatifu ya Jumapili 29/03/2015 katika kanisa la Efatha Mwenge kwa Nabii na Mtume Josephate Mwingira ibada ya pili inayoaanza saa 4:00 asubuhi na kuishi saa 7:00 mcihana. Ninaomba nikushirikishe kile nilichojifunza ili kikafanye jambo katika maisha yako

Ukiwa tishio unafanya makuu katika ufalme wa Mungu. Unatakiwa kuwa mtakatifu mahali popote. Ili uweze kuwa soko kuu mbinguni na duniani lazima uwe mtakatifu.

Ili tuweze kusherekea sikukuu na maombolezo katika ufalme wa Mungu, unatakiwa kutoruhusu unajisi bali kuwa mtakatifu mahali popote. Azimia moyoni mwako kuwa Mtakatifu mahali popote, fanya maamuzi ya kuwa kila kuitwapo leo utafanya sikukuu katika ufalme wa Mungu. Lazima ujiandae kuwa Mtakatifu kwasababu Utakatifu ni jambo endelevu

Tusome Daniel 3:1-18 Usikubali katika maisha yako kutishiwa na mtu yeyote au kitu chochote, acha kunyenyekea wanadamu kwa mali zao. Unatakiwa kuwa jasiri katika kuamua jambo na usilazimishe na mtu. La msingi ni kutii mamlaka ya Mungu na kufuata maagizo yake yote. Unatakiwa kuwa na msimamo wako kwa kufuata taratibu za Mungu na sio kulazimishwa kufuata jambo usilolipenda.

Nguvu ya Kitume inasababisha pasipo na njia kuwa na njia. Umeomba sana na ghafla mlango wa kujibiwa umefungwa, unatakiwa kuendelea kuomba mpaka mlango wako wa mafanikio utakapofunguliwa.

Bidii yako ya kuwaleta watu kanisani inatakiwa kuongezeka ili watu wakajifunze Neno la Mungu na mwisho wa siku wakaingie katika ufalme wa Mungu.

Watu wengi wanaokoka lakini kanisa haliongezeki. Watu wanaondoka kanisani kwasababu kile walichokuwa wakikitegemea kukipata hawakipati kutoakana na sisi kutokuwa na kasi ya kuwafundisha Neno la Munguna kuwatia Moyo pale wanavyopitia majaribu. Mungu akubariki


Nabii na Mtume Josephate Mwingira

SARAH KISINGI APONA UVIMBE
Namshukuru Mungu amenifanyia mambo makuu mawili, nilikuwa sijaokoka nikaja Efatha, nilikuwa nina uvimbe tumboni na nilitakiwa kufanyiwa operation, lakini Askofu wangu akasema hautafanyiwa operation Mungu ni Mwaminifu, nilipofika Kibaha nyumbani, niliendelea kuumwa sana nikapelekwa Amana Hospitali ikashindikana na nilipelekwa Muhimbili lakini baada ya kufika daktari akasema njoo tukupime, baada ya kupimwa akasema kuna jiwe kubwa sana, na akaingiza mkono akalivuta likatoka na akawaita watu waje kunipiga picha kwani mimi ni mtoto wa ajabu nimezaa jiwe, lakini nikamwambia mimi sio mtoto wa ajabu mimi ni mtoto wa Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Baada ya hapo nikaruhusiwa kwenda nyumbani.

Pia nilikuwa na kesi ya kusingiziwa, nilipotoka nyumbani kuelekea Polisi nikatamka neno nikasema Mungu mimi hii kesi sio ya kweli naomba unisaidie naingia Polisi naamini nipo na Wewe.
Mungu wa Efatha alivyo wa Ajabu, kesi ilienda hadi mahakamani lakini mawakili walianza kugombana wao kwa wao, nikaambiwa niondoke kwani kulionekana hakuna kesi walikuwa wamenisingizia kesi ya uongo. Nikaruhusiwa nikaondoka. Namshukuru Mungu wa Baba yangu Mtume na Nabii Josephat E Mwingira kwa matendo makuu Aliyonitendea.


ANASTELLA MCHOMVU APATA MASHAMBA MOROGORO
Ninamshukuru sana Mungu wa Efatha kwa ajili ya matendo makuu aliyonitendea. Wakati nakwenda Kusanyiko Kuu Kibaha Mwaka jana nilikuwa natafuta mashamba na nilikuwa natamani mashamba makubwa na nilipofika Kusanyiko Mtumishi wa Kenya akawa anafundisha somo la "Mimi ni mtu Mkubwa sana", Usiku ule nilifanya maombi na nikajibiwa usiku ule ule, nikapigiwa simu kuwa kuna mashamba Morogoro, na baada ya kutoka Kusanyiko mimi na Mume wangu tulienda Turiani Morogoro tukapewa mashamba makubwa kwa bei ya ajabu, na nilipata hekari 200 kwa ajili ya kulima, pia tumenunua hekari 10 kwa ajiri ya Efatha, na nimekuja na hati ya mauziano ya hekari 10 kwa ajili ya Efatha.

Pia Bagamoyo nimepata hekari 100, pia napenda kumshukuru Mungu kwa kunipatia Nyumba kwani jana tarehe 28/03/2015 nimefanya ibada ya kuweka wakfu nyumba yetu, Mungu wa Efatha amenifanyia maajabu.
Pia tulikuwa tumetoka kuwaona wazazi, tulipofika Tabata tulipata ajali iliyosababisha magari 4 kugongana lakini kwenye gari yetu hatukuumia, kwani nilimwambia Mungu hili gari nililiweka wakfu kwa ajili ya kazi yako.
Pia napenda kumshukuru Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira na Watumishi wote walio kuwa wananiombea.

MATUKIO KATIKA IBADA
Hongereni wote mliompokea Bwana Yesu leo, kwa nguvu yake awawezeshe wote kuishi maisha ya ushindi INAWEZEKANA kuishi maisha Matakatifu hapa Duniani. Kuanzia leo kushindwa siyo sehemu ya maisha yenu Ibilisi ameshindwa kabisa.



Comments