RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MWANAMKE SHUJAA SARAH MVUNGI ANAYEFANYA KAZI NYINGI KWA KIPINDI KIMOJA

Katika wanawake shujaa na wenye kujituma katika maisha, Sarah Mvungi ni mojawapo. dada huyu mabaye hachague kazi iliyombele yake ili mradi tu inamfaa. Mungu amempa neema ya pekee sana kwa utendaji kazi kwa haraka na kwa ufanisi. Kwa wanawake wa sasa ni ngumu sana kuona mwanamke anajituma katika kazi. Wadada wengi hapa mjini wanategemea sana wanaume au ndugu zao katika kupata mahitaji. Sarah Mvungi alipogundua kuwa yeye ni tofauti na wengine na anaweza kufanya mambo makuu alithubutu kulitendea kazi suala lake.

Hivi ninavyoongea Sarah Mvungi ni nesi, MC, mwigizaji, mjasiliamali, mwimbaji wa nyimbo za injili, mama mwenye kusaidia wenye uhitataji, mwinjilisti, kiongozi katika band ya THE UNITY, mwanamke mwenye majukumu katika kanisa lao la AKUSAMU (Amri Kumi za Mungu), mama mwenye watoto wawili, mwamamke ambaye hajaolewa. Mungu azidi kumlinda kwasababu ana mchango mkubwa katika taifa la Tanzania.

ANGALIA VIDO ZAKE KWA KUBONYEZA HAPA

Comments