RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

FLAVIANA MATATA AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUMBUKUMBU YA WALIOFARIKI MV BUKOBA

ALFAJIRI ya Mei 21 mwaka 1996 – siku kama ya leo -- ni tarehe ambayo Tanzania ilipatwa na msiba mzito ambapo zaidi ya watu 600 walifariki baada ya meli ya MV Bukoba iliyokuwa ikifanya safari zake kutoka mjini Bukoba kwenda jijini Mwanza kuzama katika Ziwa Victoria ambalo liko katika eneo la nchi za Kenya, Uganda na Tanzania.

Mwanamitindo maarufu nchini na duniani, Flaviana Matata, wakati wa msiba huo alikuwa na umri wa miaka minane, alikuwa mmoja wa waombolezaji waliofika kwenye misa maalumu ya kuwaombea marehemu waliofariki katika ajali hiyo .

Flaviana alimpoteza mama yake mzazi aliyekuwa katika meli hiyo iliyozama eneo la Bwiru jijini Mwanza ikiwa na zaidi ya abiria wapatao 800.

Misa hiyo iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mt. Francis, Nyakahoja jijini Mwanza na baadaye waombolezaji kwenda kutazama makaburi ya marehemu wa ajali hiyo yaliyopo eneo la Miti ya Nyerere, Igoma jijini Mwanza.

Akiongea katika hafla hiyo, Mwanamitindo huyo wa kimataifa amesema: “Leo ni siku ambayo sitaisahau kwani ni siku ambayo mama yangu mzazi alifariki kwa kuzama majini na meli ya MV Bukoba katika Ziwa Victoria hivyo niungane na wenzangu waliopoteza ndugu zao katika ajali hiyo ambayo ilitwaa maisha ya Watanzania wengi.”

Aidha, katika misa hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini, wasanii na vikundi mbalimbali kama Zalendo na Bongo Ride ambao wamewasha mishumaa kwenye makaburi ya marehemu yaliyoko kitongoji cha Igoma jijini Mwanza.

Matata amesema kuwa anaiomba serikali kuhakikisha kuwa vyombo vyote vya majini vinakuwa salama ili kudhibiti ajali za majini ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara.

Flaviana aliongozana na dada yake, Grace Matata, na mshindi wa Big Brother Africa, Sultan Idriss, ambaye alikuwa kivutio cha wengi katika kumbukumbu hiyo.

Waliofika kanisa katoliki la Mt. Francis, lililopo Nyakahoja-Mwanza, na kushiriki misa maalum ya kumbukumbu ya kuzama kwa meli ya Mv. Victoria. Misa ya kumbukumbu ikiendelea.


Wakifuatilia misa ya kumbukumbu.

Wakiweka mauwa kwenye kaburi.…

Baadhi ya watu waliofika katika Kanisa Katoliki la Mt. Francis, lililopo Nyakahoja-Mwanza na kushiriki misa maalum ya kumbukumbu ya kuzama kwa meli ya MV Bukoba.

Watu hao wakifuatilia misa ya kumbukumbu ya miaka 19 ya kuzama MV Bukoba.

Wakiweka maua kwenye moja ya kaburi.
Flaviana Matata akiongea neno wakati wa kumbukumbu hizo.
Sheikh akiomba dua maalum kwa ajili ya kuwakumbuka marehemu wa ajali ya meli ya MV Bukoba.
...wakipiga picha ya pamoja kwenye makaburi.
...wakipiga picha ya ukumbusho.

Comments