RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

NABII FLORA PETER: TUNAKEMEA PEPO ANAYEZUIA MAFANIKIO YAKO


NENO LA MUNGU LINATOKA KATIKA INJILI YA MTAKATIFU LUKA 9:37-43
Biblia inasema: Ikawa siku ya pili yake aliposhuka mlimani, mkutano mkubwa ulifuatana naye, natazama mtu mmoja katika mkutano alipaza sauti akasema, mwalimu nakuomba umwangalie mwanangu, kwa sababu ni mwanangu yeye wa pekee. Na tazama pepo humpagaa mara yeye hupiga kelele, tena humtia kifafa huku mwanagu hutokwa na povu, wala hamwachii ila kwa shida, hujichubua chubua.
Nikawasihi wanafunzi wako wamtoe wasiweze, Yesu akajibu akasema, akawaambia hao wanafunzi wake, enyi kizazi kisicho na imani, kilichopotoka, nitakaa nanyi nitawachukulia hata lini? Yesu akasema mlete mwanao hapa, alipokuwa katika kuenenda pepo akambwaga chini, akamtia kifafa, Yesu akakemea pepo mchafu, Yesu akamponya Yule mtoto; leo namkemea pepo mchafu anayezuia mafanikio yako, mahusiano yako, atoke kwa jina la Yesu.

JINSI YA KUFIKA KANISANI: Ukiwa unatokea Mwenge Dar es Salaam, panada magari ya Tegeta, Shuka Mbezi Mbuyuni, uliza kanisa la Nabii Flora.
MATUKIO MENGINE INGIA

Comments