RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA CHEMSHA BONGO NA BIBLE


KITABU CHA YOHANA 7

Upendo Kilahiro-Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania

Mtunzi: Rulea SangaMASHARTI: Huruhusiwi kusoma majibuwala kutumia Biblia kabla hujajibu kwa kutumia akili yako.
ONYO: Kama utaenda kinyume na masharti hapo juu utakuwa umetenda dhambi.

MASWALI

1. Kwanini Yesu hakutaka kutembea katika eneo la Wayahudi na badala yake alitembea katika eneo la Galilaya?

2. Taja jina la sikukuu ya Wayahudi

3. Kwanini Yesu alisema, “Ulimwengu hauwezi kuwachukia nyinyi, bali kunichukia mimi” ?

4. Bwana Yesu alipoamua kukwea kwenda Galilaya kula sikukuu hata kama wakati wake wa kwenda haukutimia. Je, alikwea kwa uwazi au kwa siri?

5. Kwanini watu hawakuweza kumtaja Yesu katika ile sikukuu ya vibanda iliyoandaliwa kwa Wayahudi?

6. Yesu aliwambia kitu gani Wayahudi alipokuwa akifundisha baada ya Wayahudi kustaajabu na kujiuliza kuwa Yesu amepata wapi elimu?

7. Malizia maneno haya ya Yesu, “Yeye aminiaye kwa nafsi yake tu hutafuta (i)……………………; bali yeye anayetafuta utukufu wake aliyempeleka yaani Mungu huyo ni kweli wala ndani yake hamna (ii)………………….

8. Kwanini Wayahudi walishindwa kumua Yesu alipokuwa akiwafundisha hekaluni?

9. Ni watu gani waliwatuma watumishi kwenda kumkamata Yesu?

10. Ni maneno gani Yesu alisema katika Roho siku ile ya mwisho wa sikukuu ya vibanda ya Wayahudi akiwa hekaluni?

UKITAKA KUONA MAJIBU BONYEZA "Read More" HAPO CHINI KIDOGO



MAJIBU


1. Wayahudi walitaka kumuua (Yohana 7:1)

2. Vibanda (Yohana 7:2)

3. Kwasababu Yesu alishuhudia kuwa kazi za dunia ni mbovu (Yohana 7:7)

4. Siri (Yohana 7:6)

5. Kwasababu ya kuwaogopa Wayahudi (Yohana :7….)

6. Mafunzo yangu si yangu ila ni Yake aliyenipeleka (Yohana 7:16)

7. (i) utukufu wake mwenyewe
(ii) Udhalimu

8. Kwasababu saa yake ilikuwa haijaja bado (Yohana 7:30)

9. Wakuu wa Makuhani na Mafarisayo (Yohana 7:32)

10. Mtu akiona kiu na aje kwangu anywe, aaminiye mimi kama vile maandiko yaliyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake (Yohana 7:37)

Comments