RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

SHUHUDA ZITAKAZOKUINUA KIIMANI KUTOKA KATIKA KANISA LA YESU KRISTO HUDUMA YA MAOMBEZI NA UPONYAJI KWA NABII FLORA PETER

Shuhuda hizi zilifanyika katika iada ya Jumapili 17/05/2015 katika kanisa linaloongozwa na Nabii Flora Peter. Umefika wakati wa kusoma hizi shuhuda ambazo zinaweza kukuinua kiimani na kuamini kuwa Mungu anatenda miujiza kwa kupitia watumishi wake alioweka hapa duniani

Nabii Flora Peter

SHUHUDA MBALIMBALI
MAGRETH MAGEMBE ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUACHIWA HURU BAADA YA KUDHANIWA AMEHUSIKA KATIKA TUKIO LA KUMPUGA MTU NI BAADA YA KUTUMIA STICKER YA NABII FLORA
  Bwana Yesu asifiwe, naitwa Magreth Magembe natokea kigoma;  mwezi uliopita tulipata tukio pale kwangu, tulikuwa tumelala usiku, ghafla nilisikia sauti nje watu wanakimbizana. Nikatoka nje nikafungua mlango wa ndani geti sikufungua, nikakuta mtu nje mwanaume anakisu mkononi, nikamuuliza wewe ni nani? Tulipokuwa kwenye majibishano watu wakaja wengi. Sasa wakataka kumdhuru, nikawaambia msimdhuru, tukamuuliza una ndugu yako hapa? Akasema ndio, tukamwambia tupeleke, kila anapotupeleka wanamkataa hawamjui, basi wakaamua kumpiga.

Kipindi wanampiga mimi nilikuwa nimerudi ndani kulala, sasa asubuhi nilipoamka nikakuta suruali yake ipo karibu na nyumba yangu, lakini sikujali nikawa nimeenda kazini. Kumbe jioni wale ndugu zake wamekuja na kusema mimi ndio nimesababisha ndugu yao apigwe, niliporudi tu nyumbani nikakuta nyumba imezungukwa na maaskari naambiwa nipo chini ya ulinzi, nikajiuliza nimefanya nini. Wakasema kuna tukio limetokea na nyumba tatu zinahisiwa ikiwemo ya kwako, nikaingia ndani nikawaambia watoto wangu tuombe maana shetani anajiinua, basi nikamwambia Mungu wa Nabii Flora fanya maajabu maana mimi sihusiki. Nilichukuwa sticker ya Nabii Flora nikaomba, nilipotoka nje Yule mjumbe akaniambia lakini mama wewe hauusiki, walitaka kunikamata wanipeleke kituoni Yule mjumbe akawaambia hapana, namshukuru sana Mungu wa Nabii Flora.
KAKA ANAMSHUKURU MUNGU SHAMBA LA BABA YAKE KURUDISHWA NA MTU ALIYELICHUKUWA NI BAADA YA KUPELEKA UDONGO KWA NABII FLORA NA KUOMBEWA
Bwana Yesu asifiwe
; siku ya Jumamosi mama mkwe wangu alikuwa anakwenda kunichajia simu madukani, alivyokuwa anatokea tu kwenye barabara kuu ya kwenda Tanga akamkuta Yule bwana aliyekuwa amevamia shamba la mzee anaongea na rafiki yake. Anamwambia mvua zimenyesha lakini mimi bado sijapanda kwenye lile shamba, akamuuliza umelima?

akasema ndio nimelima, akamwambia inakuaje mpaka sasa hujaenda kupanda? Akamwambia ndugu yangu yaani najisikia moyo kuwa mzito yaani sitamani kabisa kwenda kwenye lile shamba sijui hata ni kwa nini. Kwa kweli madhabahu ya Nabii Flora inatenda, kila siku zinavyozidi kuongezeka na ndivyo utukufu unavyozidi kutupandisha juu, namshukuru sana Mungu.

MWAMBANO MBELA CHUMA ANAMSHUKURU MUNGU TUMBO KUACHA KUUMA NA KUHARISHA NI BAADA YA KUTUMIA STICKER YA NABII FLORA
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Mwambano Mbela Chuma
; wiki iliyopita nikuwa nyumbani mchana nimelala nimejipumzisha tu, ghafla tumbo likaanza kunisumbua nikaanza kuharisha. Ilifika mpaka siku ya pili, ilifika hatua mpaka nikashindwa kuinukia kitandani nikawa naharisha damu, mke wangu akanishauri twende hospitali.


Nilimwambia tutaenda ila naomba tufanye maombi, basi ilifika hatua akaondoka akaja mjini mimi nilikuwa Bagamoyo nyumbani, nilichukuwa sticker ya Nabii Flora nikajiwekea tumboni nikaanza kuomba, kwa kweli tokea muda huo hali ya tumbo kuuma na kuaharisha halijauma mpaka sasa na hospitali sijakwenda, namshukuru sana Mungu.

CHRISTABELA THOMAS ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUPATA KAZI NI BAADA YA TAMKO LA NABII FLORA
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Christabela Thomas
; namshukuru Mungu wa Nabii Flora amenitendea, wiki jana nilikuwa natafuta kazi kwenye internet, nikawa nimepata Masaki nikatuma application kupitia internet. Siku ya Ijumaa nikaitwa kwenye interview, katika interview zote nilizofanya ile ilikuwa ngumu sana, kwa sababu nilipoingia tu kwenye chumba cha interview siruhusiwi kuongea kishwahili, lakini ndani ya pochi yangu nilikuwa na sticker, nikaingiza mkono nikaishika ile sticker ya Nabii Flora, nikasema Mungu nisaidie, Mungu wa Nabii Flora tenda miujiza.


Nimekaa kama dakika tatu baadaye nikajikuta naanza kuongea kingereza mpaka mwisho, nilipomaliza interview wakasema kwamba watanipigia simu siku ya Ijumaa au Jumamosi. Ijumaa wala Jumamosi sikupigiwa simu, Jumapili nipo Kanisani nikatesha kabisa simu yangu mezani nikijua labda nitapigiwa simu kwasababu walisema wanaanza kuajiri Jumatatu. Jumapili hiyo Nabii Flora alitangaza kuna watu 35 watapata ajira, nikalishika hilo neno, niliporudi nyumbani mume wangu akaniambia hebu jaribu kuwapigia namba zao si unazo, nikajaribu kuwapigia lakini hawapokei simu wanakata tu.

Jumatatu nikawa nimeshakata tamaa nikasema Jumatatu ndio wanaajiri kwa hiyo siitwi tena, muda wa saa tisa nilikuwa na mdogo wangu nyumbani nikamwambia mimi kuajiriwa ndio basi tena. Nikawa namtuma vocha nije nimpigia mama, hata kabla ya kwenda kuleta ile vocha simu ikapigwa, kuangalia ni ya kule Masaki, kupokea wakaniambia kesho Jumanne unatakiwa uje kuanza kazi niende na passport mbili na kitambulisho, kuanzia Jumanne nimeajiriwa na mpaka sasa nafanya kazi, namshukuru sana Mungu.

ELIZABETH SYLVESTER ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUPONA KATIKA HALI YA KUFA NI BAADA YA KUOMEWA NA NABII FLORA


     
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Elizabeth Sylvester; namshukuru Mungu wa Nabii Flora ameniokoa, siku ya Jumatatu nilikuwa naumwa sana nusu ya kufa, lakini namshukuru Mungu wa Nabii Flora ameniokoa.

MASAI ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUPATA NYUMBA YA KUISHI BURE NA PIA KAPATA PESA NI BAADA YA KUTAMKIWA NA NABII FLORABwana Yesu asifiwe; nilikuja kwenye maombi kwa Nabii Flora, Nabii aliponiangalia tu akasema mbona wewe ni mtu ambaye unapata pesa sana, nikasema du!


Mwenyewe sina kazi nitapata pesa wapi. Lakini Mungu wa Nabii Flora ni hatari, baadaye nilipata rafiki yangu akanipatia nyumba nakaa bure, na nikapewa kuwa kiongozi wa wamasai wote hapa Dar es salaam, na pia nimepata pesa na nimenunua ng’ombe kumi na tano, namshukuru sana Mungu.

BINTI ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUPONA UGONJWA WA KUZIMIA NI BAADA YA KUOMBEWA NA NABII
Bwana Yesu asifiwe, mimi ni mwanafunzi wa Act Open Academy
; ilikuwa siku ya Ijumaa tulipotoka shule tukapanga na marafiki zangu twende kumwona mmoja wa marafiki zangu alikuwa amefiwa na baba yake. Baada ya kutoka hapo ilikuwa muda wa saa moja usiku, nikapanda daladala kutoka Ubungo kurudi Tegeta, ghafla nilianza kusikia kichwa kinaniuma sana, nikamwambia dada aliyekuwa pembeni yangu achukuwe namba ya mama yangu endapo nitazidiwa ampigie ili kumpa taarifa.

Basi baada ya kufika Makonde ghafla nikapoteza fahamu, baada ya kupoteza fahamu kwa jinsi walivyokuwa wananielezea, mama alipigiwa simu akafika, Yule dada aliyekuwa amekaa pembeni akasema msiende nyumbani kwanza nendeni kwa Nabii Flora akafanyiwe maombi. Kweli nilipelekwa kwa Nabii Flora, nilipofika fahamu zikaanza kunijia lakini nilikuwa siwezi kuongea wala kusimama, baada ya maombi nilipona nikaondoka. Kufika nje nikamuuliza mama kwani hapa tupo wapi? Mama alisema tupo kwa Nabii Flora, nikasema jamani tumshukuru Mungu maana hilo tatizo nilikuwa nalo kwa muda mrefu. Kitu ambacho kinanifanya niamini kwamba nimepona hii hali huwa inanijia kama mtu atanishtua sana, sasa jana nilikuwa nimekaa na dada yangu ambaye ni jirani yetu tu wa kawaida, mimi huwa naogopa sana kuku, akaja akaniwekea kuku mbele yangu, nilishtuka nikawa nahisi kama vile kuna vitu vinakuja. Ghafla nikajiona tu nipo safi, namshukuru sana Mungu kwa kuniponya.

HENDRY KIWIA ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUSAMEHEWA NA MSHITAKI WAKE NI BAADA YA KUTUMIA STICKER YA NABII FLORA
Bwana Yesu asifie, naitwa Hendry Kiwia
; nilipata matatizo kazini nikasimamishwa kazi, na kabla sijasimamishwa kazi nilikuwa katika hali ya kuchanganyikiwa, sitaki kuongea na mtu wala sitaki kufanya chochote. Nilikuja kwa Nabii Flora kwa sababu walikuwa wameniletea kesi ya kusingiziwa, niliongea na Nabii Flora, nilichukuwa sticker nikarudi nyumbani, kabla ya kwenda kazini kwenye hiyo kesi mama akaniambia nichukuwe sticker. nilichukuwa sticker, nilipofika pale nikaonana na muajiri wangu akaniambia kwa jinsi wanavyoona mimi sina tatizo lolote, lakini hawezi kutoa maamuzi mpaka tukae bodi nzima pamoja na mimi na Yule mshitaki wangu.


Wakati natoka nje nikakutana na Yule aliyenishitaki akaniuliza mbona sikuoni kazini, nikamwambia ni kwa sababu ulivyonishitaki ndio nimesimamishwa kazi hadi kesi iongelewe, akaniambia yeye ameshawaambia kuwa hilo shitaka alilituma kwa makosa, kwa hiyo nitakapo rudi Jumatatu kwaajili ya kikao atawaambia kuwa alituma kwa makosa na niendelee na kazi, namshukuru sana Mungu.

MAGRETH TEMBA ANAMSHUKURU MUNGU MUME WAKE KUSHINDA KESI NA PIA MTOTO WA MDOGO WAKE AMEWEZA KUTEMBEA NI BAADA YA KUOMBEWA NA NABII FLORA
Bwana Yesu asifiwe, naitwa Magreth Temba
; namshukuru Mungu wa Nabii Flora mume wangu alikuwa anakesi kubwa ambayo ilikuwa inamfanya afungwe, alimdhamini mtoto wa kaka yangu ambaye alikuwa anaendesha magari ya mafuta ya kwenda Uganda na Burundi. Akawa ameuza gari zima ya mafuta akatelekeza gari ya watu porini, nilikwenda kwa Nabii Flora nikaonana naye, Nabii aliniuliza unataka nikuombee nini, nikamwambia mume wangu anakesi mahakamani, na pia nimefiwa na watoto wangu alafu kuna ndugu yangu ananitishia kuniua kila siku.


Namshukuru Mungu mume wangu kesi iliisha, na Yule mdogo wangu alikuwa ni mjamzito akazaa mtoto akawa hatembei, alipoona mtoto hatembea akaja akaniomba msamaha. Nikamwambia msaada kwangu upo lakini lipo neno moja tu nililipata kwa Bwana, ambalo nilienda kwa Muheshimiwa Nabii Flora ambapo hata sasa naishi kwaajili ya Muheshimiwa Nabii Flora. Yule mdogo wangu alikuja kwa Nabii Flora, akaombewa na mpaka sasa hivi mtoto wake ni mzima, anatembea na anaongea, namshukuru sana Mungu.

PENDO JOHN ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUWEZA KUWAOKOA WANAFUNZI WENZA KATIKA HALI YA MAPEPO
 Bwana Yesu asifiwe, naitwa Pendo John
; kitu kilichotokea katika shule yetu ni kitu cha kushangaza sana, tulikuwa tumekaa darasani tunajadiliana na wanafunzi wenzangu. Baada ya hapo Zulfa Machirwa akashikwa na msichana mmoja anaitwa Mariamu, aliposhikwa akaanza kuumwa na kichwa, baada ya hapo wengine wote wakaanza kupandisha mashetani.

Baada ya hapo Yule ambaye amemshika Zulfa nayeye akaanza kupandisha mapepo, mimi nikawaambia wale wanafunzi ambao wamemshika Yule embu mwachieni tuone anataka kufanya nini. Alivyoachiwa akakikmbia, alipokimbia na mimi kitu kikaniambia hebu kimbia na wewe uone kuna nini, nilipokimbia nikakuta kuna watu wawili pamoja nayeye ni mtu wa tatu wamefunga kaniki nyeusi. Nikawa najiuliza huyu anafanya nini mpaka sasa hivi wenzake wote wameshapata mapepo, akaninyooshea mikono, nikamwambia kwa damu ya Yesu umeshindwa, kama kweli natumika katika madhabahu ya Nabii Flora umeshindwa na kuna moto. Baada ya hapo nikaingia darasani nikakutana na kitu kimoja cha ajabu kina mapembe kimesimama, nikatoka nje, nilipotoka nje nikasema huyu anatuchezea tena anafanya makusudi. Waalimu wakaniambia wewe ni mwongo una nguvu za giza, nikasema hapana sina nguvu za giza, natumika katika madhabahu ya Nabii Flora, walimu wakasema acha fujo, acha uongo, nikasema sio uongo ni kitu ambacho nakiona katika ulimwengu wa Roho, wakamchukuwa Yule msichana wakamweka kwenye bajaji akapelekwa kwao. Nikawaambia kwanini Roho Mtakatifu anajidhihirisha aongee kinachotokea mnamkataza? Wakasema hapana walimu wengine wakawa wananipinga wanasema wala hatukubaliani na wewe, nikasema kama hamkubaliani na mimi mtaona kitakachotokea. Kweli nikainama chini nikaanza kuombea wale watu wambao wamedondoka chini, kweli Mungu wa Nabii Flora alijidhihirisha walipona watu wote wakanyanyuka pale chini, Mungu aliye katika madhabahu ya Nabii Flora kweli anastahili kusifiwa na kuabudiwa.

MAMA ANAMSHUKURU MUNGU KWA KUPATA MUUJIZA WA PESA NI BAADA YA KUZUNGUSHA STICKER YA NABII FLORA
Bwana Yesu asifiwe;
jana nilienda Mbezi ya Kimara kwa watoto wangu, pale huwa wanafanya biashara, katika biashara yao pale kuna bomba limekatika chini sasa likawa linamwaga maji mengi sana. Walianza kubomolewa, na mategemeo yangu ya kwenda pale ni ili niapate nauli, sasa na baada ya kubomolewa pesa hakuna. Sasa wakawa hawana pesa yakunipa, na biashara ikawa haitoki kutokana na wateja hawaji wanaogopa yale maji yaliyobomoka, nikachukuwa sticker ya Nabii Flora nikazungusha, nilipozungusha tu mwanangu mwingine wa kiume akaja akanipatia shilingi elfu sita, namshukuru sana Mungu.

Tembelea www.nabiiflora.blogspot.com
www.rumaafrica.blogspot.com
Kanisa lipo Mbezi Salasala DSM shuka kituo cha Mbezi Mbuyuni uliza kanisa la Nabii Flora..

MWISHO


Comments