RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

JENNIFER MGENDI ANAKUALIKA KATIKA UZINDUZI WA DVD YAKE NA KUMSHUKURU MUNGU KWA MIAKA 20 YA HUDUMA YAKE

Ukizungumzia waimbaji waliweza kutoa mchango wao mkubwa katika ulimwengu wa muziki wa Injili duniani na bado wanaendelea kutoa mchango wao hutaweza kumsahauJennifer Mgendi ambaye alianza kuimba akiwa bado mdogo na hivi sasa ameolewa na ana familia yake bora lakini bado yupo na Yesu. Mungu amekuwa mwaminifu kwake maana ameweza kumtendea makuu katika huduma yake ya uimbaji ikiwa ni pamoja na kuwavuta watu wengi sana kwa Yesu kwa njia ya uimbaji, pia ameweza kujulikana na watu wengi kutokana na heshima yake na uimbaji wake.

Jennifer Mgendi

Ukisikia nyimbo zake na kufuata yale anayoimba katika nyimbo zake na ukawa mtii na mtu wa kuamini, basi shida zako na tabia yako itabadilika na utakuwa na hofu ya Mungu. Kuna kitu Mungu amepanda ndani yake na kimefanyika baraka kwa watu wengi sana na kusababisha watu wengi kutamani kufanya kama yeye anavyofanya. Jennifer Mgendi ni mwanamke ambaye ni shujaa na anayejiamini kwa kila kitu anachofanya. Mbali na uimbaji pia ni mwigizaji wa filamu za GOSPEL na amekuwa akifanya vizuri sana katika kuwakilisha ujumbe wa Mungu kwa watu ili waokoke na kutambua matendo makuu ya Mungu.

Jumapili mwimbaji huyu anakwenda kuzindua albamu yake ya WEMA NI AKIBA katika kanisa la TAG DCT Tabata Shule jirani na kituo cha Polisi na hakutakuwa na kiingilio chochote. Unaombwa sana kufika ili kumuunga mkono na kumtia moyo katika zoezi zima la uzinduzi. Uwepo wako utafanyika baraka kwa wengine. Tujitokeze kwa wingi ili Mungu wetu akatukuzwe

Comments