RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MATUKIO YA TAMASHA LA FLORA MBASHA UBUNGO PLAZA KIPINDI CHA KUSHIKANA MKONO NA MH. FREMAN MBOWE KWA KUNUUNUA DVD YA "NIPE NGUVU YA KUSHINDA"

Kwa muda mrefu sana Flora Mbasha alikuwa na DREAM ya kufanya tamasha lake la uzinduzi wa DVD zake ambazo amekuwa akiziuza kwa watu wengi sana duniani na pia zimetokea kupendwa na watu wengi,  lakini wakati wa Mungu ulikuwa bado haujafika kwa mwimbaji huyu kufanya tamasha.

Flora Mbasha ni mmoja wa wakongwe wa nyimbo za Injili Tanzania na ni mmoja kati ya waimbaji wanaopendwa sana na huduma yake ya uimbaji. Watu wengi sana wamebadilisha maisha yao na wengine kuingia katika ulimwengu wa uimbaji kutokana na uimbaji wake.
Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe (kushoto) akimuongelea Flora Mbasha mazuria anayofanya kwa kazi ya Mungu.

Siku ya tarehe 14/06/2015 saa 8 mchana ndani ya Ubungo Plaza ilikuwa ni siku ambayo Mwenyezi Mungu aliiweka special kwa dada Flora Mbasha kufanya tamasha lake la uzinduzi wa video yake mpya inayoenda kwa jina la MUNGU WA AJABU. Hakika Mungu aliweza kuwatumia watu aliowaona wanaweza kumuunga mkono katika maandalizi ya tamasha lake nao ni The Fadhaget Sanitarium Clinic, Kidoti, Gombo Tours, Clouds TV, Wanawake LIVE, AG Press, ABE Sound, Coca Cola, Rumafrica na wengine wengi kudhamini tamasha lake. Pia kulikuwa na wageni waalikwa na maalumu ambao waliweza kutoa michango yao kwa moyo wa upendo.

Tamasha hili lilisindikizwa na waimbaji wengi sana kama vile Furaha Isaya, Joyce Ombeni, Lilian Kimola, Glory Mainah, Elizabeth Ngaiza, Christopher Mwahangila, Ambwene Mwasongwe na wengine wengi waliofika kumtukuza Mungu na kumuunga mkono mwimbaji wao mpendwa Flora Mbasha.

Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe ndiye aliyekuwa mgeni rasmi wa tamasha hili. Mheshimiwa aliweza kuongea maneno yenye kutia faraja na kujenga imani za watu hasa pale alipokuwa akiongelea maisha ya Flora Mbasha kwa ufupi na hasa mapito aliyokuwa akipitia. Maneno yake hakika yaliweza kumgusa Flora Mbasha na kumpa nguvu ya kusonga mbele. Mh. Freeman Mbowe aliweza kuchangia kiasi cha milioni 11 na ushehe kuidumisha huduma ya mwimbaji huyu.

Flora Mbasha aliweza kuitambulisha bendi yake  mpya ambayo atakuwa akizunguka mayo mikoani kufanya kazi ya Mungu. Rumafrica ndio walioweza kuandaa matangazo yote ya Flora Mbasha ili watu waweze kujua ni kitu gani Flora Mbasha anakwenda kukifanya, na pia kuonyesha matukio ya tamasha hilo baada ya kumalizika. Hivi leo unaona matukio haya kwa njia ya picha zilizopigwa na Rumafrica (+255 715 851 523) ili uweze kuona kazi ya Mungu aliyoifanya Flora Mbasha. Rumafrica itazidi kuwaletea tena matukio mengine ya tamasha hili.



Flora Mbasha (kushoto) akiwa na waimbaji wa bendi yake wakimsikiliza Mh. Freeman Mbowe

Flora Mbasha (kushoto)
xxxx
Mh. Freeman Mbowe

Mh. Freeman Mbowe Mwenyekiti wa CHADEMA akitoa maneno machacha kabla ya kuunza kunadi DVD ya Flora Mbasha

KIPINDI CHA WADAU WA FLORA MBASHA KUNUNUA VIDEO YA NIPE NGUVU YA KUSHINDA YA FLORA MBASHA NA KUWEZA KUSHIKANA MKONO NA MGENI RASMI MH. FREEMAN MBOWE.



MC. Sarah Mvungi (kushoto) akimsikiliza mdau wa Flora Mbasha akitamka kiasi cha kuchangia huduma ya Flora.


Mama mzazi wa Flora Mbasha akitamka kiasi cha kumchangia mwane kwa kununua DVD ya Nipe Nguvu ya Kushinda ya Flora Mbasha

Mama Mzazi wa Flora Mbasha akipokea DVD ya mwanae kutoka kwa Mh. Freeman Mbowe ambayo aliweza kujinunua
Muwakilishi wa The Fadhaget Sanitarium Clinic Bwana Lonely akitamka kiasi cha kumchangia Flora Mbasha. The Fadhaget Sanitarium Clinic chini ya Mkurugenzi Dr. Fadhili Emily waliopo Mbezi Beach Afrikana ndio wadhamini wa Tamasha hili.




Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Lilian Kimola (kushoto) akipokea DVD ya Flora Mbasha kutoka kwa Mh. Freeman Mbowe baada ya kuinunua
Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Glory Mainah akipokea DVD ya Flora Mbasha kutoka kwa Mh. Freeman Mbowe.
Meneja wa Praise Power Radio Bwana George Mpella akipokea DVD ya Flora Mbasha kutoka kwa Mh. Freeman Mbowe
Mwimbaji wa nyimbo za Injili Celline Theophile akipokea DVD ya Flora Mbasha kutoka kwa Mh. Freeman Mbowe
Mch. Maximillia (kushoto)
Furaha Isaya (kushoto) akipokea DVD ya Flora Mbasha kutoka kwa Mh. Freeman Mbowe
Furaha Isaya na Mh. Freeman Mbowe
Mwimbaji kutoka kikundi cha GWT  Bwana David (kutoto) akipokea DVD kutoka kwa Mh. Freeman Mbowe

BONYEZA "Read More" HAPO CHINI KUONA MUENDELEZO WA HAYA MATUKIO YA UUZAJI WA DVD ZA FLORA MBASHA











Mkurugenzi wa Grace Products ni mmojawapo wa  waliodhamini tamasha hili la Flora Mbasha







Lilian Kimola (kulia) na Glory Mainah ni waimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania

















Mwaimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Celline Theophile






















Mh. Freeman Mbowe (kulia) na Mch. Maximillian






Mgeni Mwalikwa akitaja mchango wake wa kununua DVD ya Flora Mbasha

Mh. Freeman Mbowe



Security


BONYEZA HAPA KUONA MAANDALIZI YA TAMASHA LA FLORA MBASHA