RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

NABII NA MTUME JOSEPHATE MWINGIRA WA KANISA LA EFATHA MWENGE AFUNDISHA JINSI YA KUMGOJA BWANA KATIKA IBADA YA JUMAPILI

Jumapili ya tarehe 12/07/2015 Rumafrica ilibahatika kufika katika kanisa la Efatha lililopo Mwenge jijini Dar es Salaam na kuhudhuria Ibada ya pili inayoanza saa 4 asubuhi na kumalizika saa 7 mchana. Ibada hii ilikuwa ni ibada ya kumsifu Mungu kwa njia ya uimbaji. Mtume na Nabii Josephate Mwingira aliweza kutoa Neno la Mungu kwa ufupi, na hivi ndivyo ilivyokuwa

Picha ya Nabii na Mtume Josephate Mwingira katika ibada za mikoni

Bwana Yesu Asifiwe, Tusome Zab:40. Ni wakati gani wanafika wakati wanamuogopa Mungu wako? Ni pale unapokuwa uko katika hali ya kumngoja Bwana. Hali yako ya kujitoa ndiyo inayoitwa hali ya kumngoja Bwana, fanya kitu kinachosubiri yeye Bwana aje.Unapotaka kumngoja Bwana fungua mlango ili Bwana aingie, au fanya jambo litakalosababisha Bwana afurahi. Hata kama upo kwenye mfungo andaa nyimbo zako, na uiimbe kwa furaha bila kujali njaa inayokuuma kipindi umefunga.

Fanya kitu unachotarajia huko ndiko kumngoja Bwana. Lazima ujue muda wa kumngojea Bwana. Uimbaji wako unaweza kusababisha watu kumpenda Mungu. Wakati mambo yamekuharibikia fanya jambo la kumgusa Bwana na kumshtua Bwana.

Unatakiwa kuwa na imani ya juu sana, jitamkie maneno ya mafanikio na ukishatamka amini yamekuwa. Tenda mema na watu wanavyokusimulia wewe, tambua habari zako zinaenea na Kristo anakuwa amewafikia watu wengi. Jitahidi kuongea vizuri kuhusu habari zako ili Mungu afanye sawasawa na habari zako. 



Comments