RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ASKOFU MH. DKT. GERTRUDE RWAKATARE WA KANISA LA MIKOCHENI B ASSEMBLIES OF GOD MLIMA WA MOTO AZINDUA RASMI KANISA JIPYA LA MLIMA WA MOTO KIGAMBONI JIJINI DAR ES SALAAM

Siku ya Jumapili 28/08/2015 Askofu Mh. Dkt. Gertrude Rwakatare baada ya ibada aliweza kufika Kigamboni Gezaulole kuzindua rasmi kanisa jipya la Mlima wa Moto Kigamboni. Siku hii ilikuwa ni siku ya kumshukuru Mungu kwa matendo makubwa aliyoyafanya katika kanisa la Mlima wa Moto kwa kufanikisha kupata kanisa jipya ambalo litasaidia sana kuwaleta watu kwa Yesu na pia kuwainua wakazi wa Kigamboni kuishi katika maisha ya kumtumainia Bwana.

Askofu Mh.  Dkt. Gertrude Rwakatare akimshukuru Mungu

Askofu Mh. Dkt. Gertrude Rwakatare ambaye amekuwa na kilio cha kuwainua watu KIROHO na kuwapa upako wa kutamani kufanya kazi ya Mungu, amekuwa msaada mkubwa sana kwa Watanzania na hivi sasa matokeo yanazidi kuonekana machoni pa watu. Kipindi cha nyuma tuliona alivyoweza kulifungua rasmi kanisa la Boko jijini Dar es Salaam ambalo kwa hakika limekuwa likiwasaidia wakazi wa Boko kuishi katika maisha ya kumtumikia Mungu na kuwa na hofu ya Mungu.
Askofu Mh.  Dkt. Gertrude Rwakatare akiaangalia mazingira ya kanisa

Katika kanisa hili jipya la Mlima wa Moto Kigamboni tunategemea makubwa kuyaona kwa wakazi wa Kigamboni na sehemu za jirani ambao watakuwa wakiabudu mahali hapo. Mungu atakwenda kuwainua wakazi hawa Kiroho na kimwili. Askofu Dkt. Gertrude Rwakatare ni kati ya watumishi wa Mungu ambao Mungu wa mbinguni amewapa neema ya kuwasaidia watu kuinuka kiuchumi na hasa Kiroho. Watu wamekuwa wakitoa shuhuda zao jinsi Mungu alivyowainua kiuchumi baada ya kukanyaga katika nyumba ya Bwana na kuombewa na Askofu huyu.
 Kanisa la Mlima wa Moto Kigamboni litakuwa ni kituo cha miujiza, ishara na pia kitovu cha Neno la Mungu kwani kutakuwa na wachungaji ambao Mungu mwenyewe atakuwa anawatumia kupeleka ujumbe wake kwa watu
 Askofu Mh.  Dkt. Gertrude Rwakatare (kulia) na Mch. Noah Lukumayi (katikati)






 Mwimbaji wa nyimbo za Injili na mjasiriamali David Robert

Askofu Mh.  Dkt. Gertrude Rwakatare
 David Robert





 BONYEZA "READ MORE" HAPO CHINI KIDOGO KUSHOTO




David Robert