RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

LOWASSA AMBAYE ALISHAWAHI KUONGEA NA NABII TB JOSHUA AZIDI KUWATEMBELEA WANANCHI DAR


MGOMBEA wa urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Ngoyai Lowassa kwa mara nyingine ameendelea na ziara yake ya kujua matatizo ya wananchi kwa kuwatembelea wananchi mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam ambapo leo aliwatembelea wafanyabiashara ndogondogo kwenye Soko la Tandale na Tandika. Katika ziara hiyo ambayo ilikusanya umati wa watu, Lowassa alianzia katika Soko la Tandale ambapo alipofika alipokelewa na wafuasi wa Chadema waliosikika wakiimba wimbo wa kumsifia Lowassa kwa kumuita ‘rais wa wanyonge.’ Akiwa sokoni hapo, Lowassa alizungumza na baadhi ya wafanyabiashara wa mahindi ambao walimueleza changamoto za biashara yao lakini wakasema wanaamini kama wananchi wote wataamua kumpa ridhaa ya kuwa rais, atawaboreshea mazingira ya bishara yao. Baada ya kuzungumza na wafanyabiashara hao katika Soko la Tandale, msafara wa Lowassa ulihamia katika Soko la Tandika lililopo Manispaa ya Temeke, jijini Dar kujionea changamoto wanazokutana nazo wafanyabishara. Mara baada ya kumalizana na wafanyabiashara wa Tandika, kiongozi huyo alielekea Soko la Kariakoo ambako alikutana na polisi ambao walimzuia kwa kumueleza kuwa ziara yake haikuwa rasmi hivyo inaweza kuhatarisha usalama wa raia. Jana, Lowassa aliianza ziara hiyo kwa kutembelea maeneo ya Gongo la Mboto kwa kutumia usafiri wa daladala ili kujua kero za wasafiri. 



Mgombea urais, Edward Lowassa (katikati) na mgombea mwenza Duni Haji (kulia kwa Lowassa) kupitia Chadema/Ukawa wakiwa katika soko la Tandale jijini Dar kuwatembelea wafanyabiashara.


Lowassa akisalimiana na bibi muuza mbogamboga soko la Tandale.


...Akiongea na muuza chai.

Wafanyabiashara wakiwa wamezunguka gari lilombeba Lowassa (katikati).


Lowassa (katikati) na Duni Haji wakiwaaga wafanyabiashara.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala Lucas Mpondya (kushoto) akijadiliana jambo na askari wake mbele ya gari la waandishi wa habari lililokuwa likitumiwa kwa shughuli ya ziara ya Lowassa.

PICHA: HARUNI SANCHAWA/GPL

Comments