RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MATUKIO YA UZINDUZI WA BONY MWAITEGE..MSANII WA BONGO MOVIE LULU AHUDHURIA

Binafsi nimefurahi sana kuona Elizabeth Michael (Lulu) kuhudhuria katika matamasha ya Gospel. Lulu ni msanii mkubwa sana Tanzania katika ulimwengu wa filamu za Kibongo yaani Bongo Movie. Msanii huyu ambaye ametokea kujulikana tangia akiwa mdogo sana katika uigizaji ameweza kuwapata wapenzi wengi sana wanaopenda kazi zake. Kitu kingine kilichonifurahisha kutoka kwa Lulu ni pale tu alipoweza kucheza na kufurahi na Watanzania wenzake huku akionyesha kukuubali uimbaji wa Bony Mwaitege. Lulu alijikuta akivutiwa sana na mwimbaji wa nyimbo za Injili Ambwene Mwasongwe kwa uimbaji wake, hii ilimfanya amfurahie na aliweza kumfuata na kufanya naye mazungumzo naye kidogo na kupokea upako kutoka kwa Ambwene.














Siku ya Jumapili ilikuwa siku ya kipekee sana kwa mwimbaji wa nyimbo za Injili Bony Mwaitege alipokuwa akizundua DVD yake ndani ya ukumbi wa Diamond jijini Dar es Salaam. Tamasha hili liliweza kuwakusanya watu wengi sana wakiwemo Watumishi wa Mungu, wasanii wwa Bongo Movie, waimbaji wa nyimbo za Injili na watu mbalimbali. Tamasha hili likuwa na mvuto wa kipekee. Uimbaji wa Bony Mwaitege uliwagusa watu wengi sana na hasa mavazi yake yalitokea kupendwa sana.

Bony Mwaitege ni mwimbaji mkongwe Tanzania na ni mwimbaji mwenye kupendwa sana na watu wengi kwa uimbaji wake na kucheza kwake.

Lulu akifanya yake

Lulu akipokea upako kutoka kwa Ambene Mwasongwe wakati akiimba stejini

Kutoka kulia ni mwimbaji wa gospel Upendo Kilahiro, Lulu na Ambwene Mwasongwe

Lulu akiwa na Ambwene Mwasongwe
 
Lulu akiwa na Emmanuel Mbasha




Picha kwa hisani ya Uncle Jimmy

BONYEZA "Read More" HAPO CHINI KIDOGO-KUSHOTO KUONA MATUKIO MENGINE YA TAMASHA HILI LA BONYY MWAITEGE










Munishi kutoka Kenya alikuwepo akifanya kweli jukwaani.

 
Lulu akiwa na Mama yake mzazi siku ya jana….hapa akicheza kwa furaha baada ya kumuona Ambwene Masongwe jukwaani.

Ambwene akiokota pesa alizotunzwa na mashabiki wake….







Comments