RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MKESHA MKUBWA WAFANYIKA NYUMBANI KWA MASANJA MKANDAMIZAJI

Hii inaleta matumaini kwa vijana wenye nia na usongo wa kumtumikia Mungu mali zao na akili zao. Mchungaji mtarajiwa kama anavyojiita, Emmanuel Mgaya (Masanja Mkandamizaji) aliweza kuaandaa mkesha nyumbani kwake Barakuda Tabata jijini Dar es Salaam. Mkesha huu ulihudhuriwa na watu mbalimbali kuja kumtukuza Mungu. Vijana wengi waliweza kufika na kuweza kusikia ujumbe kutoka kwa Mch. Mtarajiwa Masanja Mkandamizaji.

Mchungaji huyu ambayo ameanzisha huduma yake inayoitwa STREET GOSPEL INTERNATIONAL akiongea na Uncle Jimmy aliweza kusema hivi sasa ameanza huduma hii ya kumtumikia Mungu nyumbani kwake lakini baadae ataweza kuanza kufanya mitaani na vijini. Watu wengi wamekuwa wakisema mchungaji huu anatania kuwa mchungaji kutokana na ucheshi wake na  kuchekesha kwake, lakini yeye amekili kuwa ana maanisha kwani anajua ni wapi Yesu Kristo amemtoa. Na hii huduma yake itakuwa inafanyika kila mwisho wa mwezi ambapo watu watapata chakula cha rohoni kwa njia ya sifa na Neno la Mungu

Tuone matukio katika picha zilizopigwa mida ya saa saba usiku




Watu mbalimbali wakifatilia neno kutoka kwa Emmanuel/Masanja Mkandamizaji.






BONYEZA "READ MORE" HAPO CHINI KIDOGO KUSHOTO KUONA MATUKIO MENGINE YA MKESHA HUU.




Huyu Baba sio bure kunakitu kina furukuta ndani yake……

Akichapa injili mdau wangu

Kama uonavyo hapa ni juu ya Gorofa.








MC Joshua Makondeko alikuwepo.

Comments