Picha kwa hisani y Rumafrica +255 715 851 523
Jumapili hii ilikuwa ni jumapili ya baraka sana kwa watu Mungu waliofika katika kanisa la Mlima wa Moto Assemblies of God. Ibada hii ilipambwa na uimbaji malidadi kutoka katika kwaya za hapo kanisani. Watu waliweza kumsifu Mungu wetu wa mbinguni.
Mchungaji Kiongozi wa kanisa hili Mh. Dkt Getrude Rwakatare kwa kumtii Mungu wetu aliweza kuleta ujumbe Munu kwa waumini wa kanisa hilo. Watu walionyesha kuguwa sana mahubiri ya mchungaji. Pia aliweza kuwaombea watu wenye uhitaji na kukemea mapepo yaliyokuwa yakiwasumbua kwa muda mrefu. Watu waliweza kumiminika madhabahuni huku wakiwa wamebebwa hawajiwezi na kupelekwa kwa mchungaji Dkt. Getrude kuombewa. Mungu aliweza kukata vifugo vya mateso yao kwa kupitia maombezi yaliyokuwa yakiendeea hapo kanisani.
Wageni kutoka Marekani ambao waliweza kupata nafasi ya kuhubiri nma kumtukuza Mungu wa mbinguni. Wageni waliweza kumpongeza Mch. Dkt. Getrude Rwakatare kwa kazi nzuri anayofanya kwa jamii kwa kuwaongoza kufika mbinguni kwa Baba wetu wakiwa watakatifu. Walishangazwa sana kuona watu wengi wamekusanyika pamoja kanisani wakiwa makini kusikiliza Neno la Mungu kutoka kwa watumishi wa Mungu ambao walikuwa wakihubiri mahali hapo.
Watu wengi waliweza kuokoka na kukataa maisha ya zamani waliyokuwa wakiishi kwa kuteswa na nguvu za shetani. Watu hao waliona kumrudia Yesu Kristo kuna faida kubwa sana na ndio maana waliamua kujiunga na kanisa hili.
Wageni kutoka Marekani waliweza kupata muda wa kuwaonyesha waumini wa kanisa hili matendo makuu ya Mungu ambayo wamekuwa wakifanya nchi mbalimbali ambazo wamebahatika kufika ikiwemo Somalia. Pia waliweza kushuhudia jinsi gani Mungu amekuwa mwaminifu kwao wanapokuwa wanahubiri katika nchi ambazo haziamini Ukristo, wamesema Mungu amekuwa mwaminifu kwao na wameweza kuwa marafiki wa watu hao wasioamini Ukristo.
Pia waliweza kufundisha jinsi ya kutunza ndoto yako. Walisema, unatakiwa kuitunza ndoto yako mpaka imetimia, hutakiwi kukata tamaa unapopitia magumu na ukasababisha kupoteza ndoto yako, unatakiwa kuishikikiria ndoto yako mpaka itimie. Ukimwamini Mungu kwa uaminifu naye atakusaidia kutimiza ndoto yako. Hakikisha kila wakati unaikumbuka ndoto yako na unatakiwa kufanya juhudi za kuhakikisha ndoto yako inatimia.
Hapa wakingalia mtendo makuu yaliyotokea Somalia
Mch. Getrude Rwakatare wa tatu kutoka kulia akiangalia clip ya mgeni wake kutoka Marekani alivyoweza kufanya kazi ya Mungu Somalia na viziwi walipona
Mch. Dkt. Getrude Rwakatare akiwa katika maombi
Mch. Dkt. Getrude Rwakatare akiwa katika maombi
BONYEZA "READ MORE" HAPO CHINI KUONA MATUKIO MENGINE
BONYEZA "READ MORE" HAPO CHINI KUONA MATUKIO MENGINE
Mch. Lukumayi
Comments