RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KIBAO KIPYA CHA MOYO WANGU HAUNA WOGA CHA MESS JACOB CHENGULA NI TISHIO

Mess Chengula ni mwimbaji pekee mwenye kipaji tofauti sana katika uimbaji wake, ni mwimbaji ambaye huwezi kufananisha na waimbaji wengine kuanzia sauti na uchezaji wake. Mungu amempa neema ya kuwa na moyo huruma na upendo kwa watu na hasa kwa waimbaji wenzake na watumishi wa Mungu.

Hivi sasa ameachia nyimbo zake mpya katika vituo vya redio akiwashirikisha waimbaji maarufu sana kama Upendo Nkone. Hakuna mtu asiyemjua Upendo Nkone kwa uimbaji wake na hivi sasa ameweza kufanya kolabo na mwimbaji machachari Mess Jacob Chengula.


Mess Chengula

Si kila mwimbaji maarufu wa Gospel yuko tayari kufanya kazi na mwimbaji mwenzake hapa duniani, lakini kutokana na uimbaji mzuri wa Mess Jacob Chengula, Upendo Nkone akaoina ni vizuri kushirikiana na mwimbaji huyu ili kuleta kitu kizuri kwako wewe msikilizaji na mtazamaji upate baraka za Mungu kupitia sauti hizi nyororo.

Mess Jacob Chengula (kushhoto) na Upendo Nkone

Mungu amembariki kuwa mfanyabiasha mkubwa sana jijini Dar es Salaam katika usambaji nauuzaji wa vifaa vya pikipiki Kariakoo jumla na rejareja. Mbali na kuwa busy na biashara lakini amekuwa akitenga muda wake kwaajili ya kazi ya BWANA. Kuna baadhi ya waimbaji wakibarikiwa au wakioa au kuolewa husahau kufanya kazi ya Bwaana, lakini hili limefanyika tofauti kwa mwimbaji huyu ambaye ameoa lakini bado kila kukicha anawaza juu ya kufanya kazi ya Mungu.

Mess Chengula akiongea na Rumafrica kwa njia ya simu kuhusu ujio wake mpya wa uimbaji wake amesema anamshukuru sana Mungu kwa upendeleo aliofanya kumuunganisha na waimbaji maarufu Tanzania kufanya nao kazi, hakika wamembariki sana kwani kazi waliyoofanya kwaajili ya utukufu wa Mungu ina mguso mkubwa sana na imekubarika na jamii. Masi tuzidi kumuombea Mess Jaco Chengula katika huduma yake ya uimbaji.



Comments