Jina langu la lililoko
katika cheti cha kuzaliwa ni Rulea Sanga, niliyezaliwa Makete miaka mingi iliyopita, na baada ya hapo mama yangu ambaye
kwa sasa ni marehemu alikuja kuhamia katika kijiji cha Mtili "A"
ambako mimi na mama yangu tukaweka makazi yetu hapo.
Namshukuru kaka yangu Marehem Amir Sanga, alinipeleka shule ya msingi na kuanza
masomo yangu mwaka 1988 katika shule ya Msingi Mtilia "A". Nakumbuka siku ya kwanza napelekwa niliingizwa katika
ofisi ya Mwalimu Mkuu Kondo na kuandikishwa. Nilionyeshwa darasa langu na baada
ya siku chache nilichanguliwa kuwa Kiongozi wa darasa (Monitor) kwahiyo kazi
yangu ilikuwa kusimamia kazi zote za wanafunzi wenzangu wa darasa na pia
kuwapelekea madaftari yao
kwa walimu ili yasahihishwe.
Katika uongozi wangu huo nilichukia sana kazi ya
kuandika majina ya wapiga kelele kwani kulikuwa na lawama sana
na kulikuwa na watu wenye nguvu ambao ukiandika majina yao tu, ujue siku yako mitaani itakuwa mbaya.
Nakumbuka siku moja nilimwandika dada mmoja anaitwa Bety, dada alikuwa na ubavu
sana, baada ya
kumuandika aliadhibiwa na mwalimu. Bety siku moja nikiwa natoka darasani
kueleka nyumbani alinishika shati na kunitwanga kichwa katika mdomo wangu, na
mdomo wangu kupasuka pale pale, nililia sana…Nilipofika nyumbani nikiwa
nimepasuliwa mdomo niliogopa kumwambia mama yangu kwani niliona aibu kusikia
nimepigwa na mwanamke, nilimdanganya mama yangu, lakini baadae alikuja kujua
chanzo cha kupasuliwa kwa mdomo wangu. Mama alinihudumia na baadae nilipona. Na
mpaka sasa nina kovu lake.
Nilipofika darasa la tatu nilikuwa ni mtu mwenye wivu sana katika masomo. Sikuwa mtu mzuri sana kimasomo lakini
nilitamani kuwa mtu wa kwanza katika masomo. Darasani kwetu kulikuwa na watu
waliokuwa akili sana, na baadhi yao ni Chesco Sanga (mtoto wa pili wa kaka
yangu wa kwanza katika familia yangu), Christina Komba, Rehema Komba, Kaja
Mtavangu, Shida Mahenge (huyu ni dada ambaye alikuwa tishio darasani), hawa
ndio walioonekana kunisumbua sana. Lakini mimi nilikuwa nashinda sana na mtoto wa kaka
yangu, Chesco Sanga, sikutamani aonekane ananishinda kimasomo. Namshukuru Mungu
hawa watuwalinisaidia sana
kuinuka kimasomo.
Kuna wanafunzi waliokuwa madarasa ya juu yangu ambao walikuwa na akili sana na walikuwa
wakizawadiwa kila mwisho wa mwaka kwa kupewa daftari na kalamu, watu hao ni
Musa Mtambalike, Tadeo Sanga (mtoto wa mjomba wangu), Marehemu Emilio Mbilinyi.
Nilitamani sana kuwa kama wao nah ii
ikanisababishia mimi kusoma kwa juhudi sana.
Kipindi tunasoma tulikuwa hatuna tuition wala muda wa kujisomea tukitoka
darasani. Mara nyingi mwalimu anapokuwa darasani ndipo tunakuwa makini katika
kusoma au pale mwalimu anapotupa muda wa kujisomea. Tukirudi nyumbani
tunaachana na masomo na kufanya kazi za nyumbani kama
kuchota maji, kukata kuni msituni, kulima na kazi zingine nyingi. Maisha hayo
yalikuwa ya kawaida sana na hakuna mtu aliyekuwa
anashangaa juu ya hilo.
Nilipofika darasa la sita nilichanguliwa kuwa mtunza muda au mgonga kengere .
Wajibu wangu ulikuwa kugonga kengere ya saa 1 au 12 asubuhi ili wanafunzi waweze
kuhesabiwa namba, kugonga kengere za vipindi, kugonga kengere kwaajili ya
kuwaruhusu wanafunzi kwenda nyumbani. Wanafunzi walionekana kuchelewa walipewa
adhabu kama kupigwa viboko, kulima mashamba,
kuleta mzigo wa nyasi na adhabu nyingine nyingi.
Nilichukia sana kazi hii kwani
ilikuwa inanilazimu kuamka asubuhi na mapema, na kuwepo shule muda wote kwani
sikuweza hata kutoroka.
Kuna marafiki zangu ambao sitawasahau kama vile Nasa, jamaa huyu ni moja ya
wanafunzi waliokuwa watoro sana
shule, alikuwa anashinda msituni akiwinda. Pia kuna rafiki yangu Paskari
Cahaula, huyu alikuwa naye mtoro sana na mgomvi sana, wanafunzi tulikuwa tukimuogopa sana kutokana na ukatili wake.
Kuna michezo Fulani ambayo ilikuwa ikinifurahisha sana nikiwa shule ya msingi. Tulikuwa
tukiwakamata wasichana na kuwalaza chini na sisi kuwaangukia juu, na hii
ilikuwa ikifanyika wakati wa kwenda nyumbani baada ya masomo kuisha. Tulikuwa
tunaweka kioo chini ya miguu ya wadada na kuwachungulia.
Nawakumbuka walimu wangu waliokuwa wakinifundisha nikiwa darasa la kwanza; Mwalimu Mlula (alinifundisha Kiswahili) , Marehemu Mwalimu Mpiluka (alinifundisha Mwandiko na Hesabu). Kuna walimu wengine walionifundisha kuanzia darasa la pili mpka la saba ambao ni Mwalimu Mkuu Kondo na baadae alihama nakuja Marehemu Mwalimu Mkuu Ndelwa, Marehemu Mwalimu Mveyange ambaye alikuwa mlemavu wa mguu mmoja, Marehemu Mwalimu Namanga, Mke wa Mwalimu Ndelwa (alinifundisha Sayansi), Mwalimu Onesmo (alinifundisha Jiografia), Mwalimu Rashid (alinifundisha hesabu), Mwalimu Mpinda (alinifundisha Michezo) na wengine
Nakumbuka nikiwa kijijini hapo, nimelima sana, nimewinda sana, na shughuli nyingi unazozijiua za vijijini. Nakumbuka wakati wa jumamosi nilikuwa naongozana na rafiki zangu kama Hadija Chaula, Ombeni Sanga, Rashid Chaula, Mashaka, George Sanga, marehemu Silvatus Mtavangu, na wengine wengi tunaelekea katika mto mmoja ulikuwa unaitwa Mbalue kufua nguo. Kutoka katika makazi mpka kufika katika mtu huo ni mbali kidogo, kwahiyo usafiri wetu ulikuwa ni baiskeli na mbao “Vigereti” au troli za mbao.
Basi tukifika mtoni hapo,
sabuni tuliyokuwa tunatumia ni majani yaliyokuwa yanaitwa “majani ya mtavangu”.
Majani hayo ukiweka kwenye maji na kufikicha yanatoa povu. Tulipenda sana kuongelea katika mto ule, na bila kuogopa nyoka za
majini hata kama kuna siku zingine zilikuwa
zikionekana.
Niliyafurahia sana
maisha yale, kwani kulikuwa na hali fulani ya upendo kati yetu. Mbali na kufua
nguo zetu, pia kulikuwa na shughul zingine nilizokuwa nikifanya na rafiki zangu
hasa kipindi cha wikendi. Tulikuwa tunafunga safari kwenda kununua matunda damu
katika kijiji cha Ikonongo na umbali mkubwa sana, na hatukuwa tunatumia usafiri wowte
zaidi ya kutembea kwa miguu. Matunda hayo tulikuwa tukiyanunua na kuyauza.
Kuna baadhi ya kazi tulizokuwa tukiwa tunasoma na zilitokea kunikera sana. Baadhi ya kazi hizo
ni kulima mashamba ya shule, kufanya vibarua vya shule kwa kulima au kupalilia
miti au mhindi katika mashamba makubwa kama ya
marehemu Mlumbe, Marehem Lusan Sanga (mjomba wangu), mashamba ya chai ya Itona
(kuchuma chai) na mashamba ya watu wengine. Tulikuwa tunashinda mashambani
kuanzia asubuhi hadi jioni. Kuna siku zingine tunaingia shambani jioni. Kazi
hizi nilizichukia sana.
Nikiwa bado darasa la sita, nilichaguliwa kuwa mmoja wa wasaidizi wa Mapadre
ambao walikuwa wakitokea Parokia ya Mafinga na kuja kuhubiri kanisani kwetu
Mtili “A”. Niliipenda sana ile kazi kwani
nilikuwa karibu sana
na Wazungu na Wahindi. Kijijini kwetu kuwa karibu na mzungu ulionekana mtu wa
maana sana.
Namshukuru sana
Katekista Kalinga ambaye kwa sasa ni marehemu. Tulikuwa tunasaidiana na motto
wa katekista Fredy Kalinga ambaye na yeye ni marehemu. Tulipenda sana na Fredy na baba yake
alitokea kunipenda kutokana na tabia yangu nzuri mbele za watu.
Nilipofika darasa la saba nilijiibidiisha sana kimasomo, nilitamani sana kusoma. Kuna vitu vilikuwa ninanikera sana katika elimu yangu. Nikiwa nyumbani sikuweza kusoma usiku kutokana na kukosa taa ya kusomea, nikibahatika nilikuwa natumia kibatali ambacho kilikuwa kikitoa moshi mzito sana, na chumba kinajaa moshi.
Siku moja kaka yangu Amir
sanga ambaye ni marehemu aliona ile hali hakupendezewa na kuahidi kuninunulia
taa ya chemli, na hii ilinisaidia sana
kwani nikawa sipati moshi kabisa. Kijiji nilizidi kuheshimika kwani ni watu
wachache wanaotumia taa ya chemli.
Siku ya mtihani wa darasa
la saba ulipofika, Mwalimu namanga na Mwalimu Mrs. Ndelwa (mke wa mwalimu mkuu)
walikuja ghetoni kwangu usiku na kuniambia siku ya mtihani nisihofu sana na
nisipaniki, maana walijua hali yangu na bidii zangu katika masomo. Siku ya
mtihani ilipofika nilifanya vizuri na ninamshukuru sana Mungu nilifaulu na kujiunga na shule ya
sekondari ya Njombe mkoani Njombe.
Inaendelea...
MAISHA YA SHULE NIKIWA SHULE YA SEKONDARI NJOMBE.
RULEA SANGA KIPINDI YUKO SHULE YA SEKONDARI NJOMBE (NJOSS) 1995-1998 KIDATO CHA KWANZA HADI CHA NNE
Rulea wa pili kutoka kushoto nikiwa Mbeya kipindi cha likizo
Rulea Sanga niliyevaa sandos nikisoma bwenini
Rulea Sanga kushoto nikiwa na kikundi cha Tambaza. Kutoka kulia ni Allen Mwihava, wa tatu ni Nasoro, Tryphone na Embagise
Rulea sanga kulia nikiwa na rafiki yangu niliyempenda sana shuleni
Rulea sanga nikiwa na marafiki zangu, kulia ni Samy ambaye kwa sasa ameokoka, Yusuph
Nikiwa Disko
Rulea sanga katikati katika mapozi..Mungu anisaidie
Rulea sanga wa pili kutoka kushoto nikiwa na rafiki zangu Mbeya kipindi cha likizo
Rulea Sanga wa pili kushoto nikiwa na rafiki zangu wa kidato cha pili
Rulea Sanga wa tatu kutoka kushoto nikielekea mjini kuzurula wakati wenzangu wako darasani
Rulea Sanga wa pili kutoka kulia nikionyesha mapozi ya mamtoni, na rafiki zangu wa Tambaza
Kutoka kushoto ni Fikiri, Simon (niga), Deo ambaye alipata Division One, Rulea Sanga
Rulea Sanga wa pili kutoka kulia nikiwa na class mate zangu. Kulia ni Samy Black
Rulea Sanga kulia, nikiwa najisomea na rafiki yangu Fadhili Rwendo ambaye sasa hivi ni Mwanashera (Wakili)
Rulea sanga wa pili kutoka kushoto, wakati wa gradution yangu kidato cha nne
Rulea sanga nikiwa katika gari la Marehemu kaka yangu Amir Sanga maeneo ya Mafinga Iringa wakati wa likizo
Nikipata chakula cha jioni katika Dinning Hall NJOSS
Rulea Sanga wa tatu kutoka kushoto nikiwa na kundi la Tambaza
Rulea Sanga, kulia nikiwa na wadogo zangu wa kidato cha pili, wakati mimi nikiwa kidato cha tatu
Rafiki yangu Tryphone ambaye aliruka na Division One kidato cha nne wa kwanza kulia
Nikiwa katika bustani yangu-NJOSS
Kikundi kutoka Tambaza
Rulea sanga wa pili kutoka kushoto nikiwa kidato cha pili na classmate wangu
Nikiwa kidato cha nne, niliyechuchumaa
ANGALIA PICHA
ANGALIA PICHA
Rulea Sanga ndani ya Mafinga mkoa wa Iringa maeneo ya Mkombwe
Rafiki
yangu niliyempenda sana wa kitaa, anaitwa Sebastian. Huyu jamaa alikuwa
kichwa sana Chuo Kikuu ila watu walimchezea akawa chizi. Ila kiingereza
usimguse
Nikiwa kanisani Mafinga kipindi cha likizo, niliyechuchumaa
Katikati ni Rulea sanga nikiwa na rafiki zangu, Tryphone (kushoto) na Sanjigwa
Nikiwa katikati na classmate, kushoto ni Onesmo Mhewa ambaye aligonga Division One kidato cha nne
Nikipiga Basketball
Rulea Sanga nikivalishwa taji wakati wa garaduation yangu ya kidato cha nne. Kushoto ni Timoth
Rulea nimkiwa katika pozi ambalo silielewi kiukweli
Rulea sanga kulia nikiwa bwenini na David Mhonzo
Rafiki yetu alitutoka shuleni Njombe na kupelekwa kuzikwa kwao Mbeya
Nikiwa maeneo ya Mafinga sokoni na rafiki yangu kipindi cha likizo
Nikiwa disko katika ukumbi wa shimoni kwa No Sweat Mafinga kipindi cha likizo
Rulea Sanga aliyevaa kofia akiwa na marafiki zake wakifanya pikiniki mkoani Njombe. Kulia ni classmate David
Rafiki zangu wakiwa bwennini namba 5. Asili yao ni watu wa Mbeya. Sam (Panagamawe) kulia
Nikiwa Disko Mafinga katika ukumbi wa hospitali ya Mafinga kipindi cha likizo
Kulia ni Rulea Sanga na David Muhonzo
Rulea kulia nikiwa na rafiki yangu (mtalaamu wa mpira wa kikapu). Tupo dukani kwa marehemu kaka yangu Amiri Sanga Mafinga Iringa
Rulea Sanga nikiwa katika korido karibu na darasa langu. Nyuma yangu ni Justin Sanga
Rulea Sanga katika pozi katika korido la darasani kwangu Njombe (NJOSS)
Kulia ni rafiki yangu niliyempenda sana shule nzima Michael Mtweve
Rulea Sanga kushoto na Justin Sanga mkoani Njombe shuleni NJOSS
Rulea Sanga na David Muhonzo mkoani Njombe (NJOSS)
Rulea Sanga (kulia) na mtoto wa kaka yangu Daniel Sanga
MAISHA YA HIGH LEVEL KATIKA SHULE YA JITEGEMEE MGULANI DAR ES SALAAM
Kulia ni Rulea Sanga na classmate wangu
Rulea Sanga wa pili kutoka kulia nikiwa na Simon, Omary Kaseko ambaye kwa sasa anaishi Marekani
Rulea
Sanga (kushoto) nikilishwa keki na rafiki yangu Japhate katika siku ya
kuzaliwa ya rafiki yetu baada ya kumaliza kidato cha sita, kipindi hiki
nilikuwa naishi kwa huyu rafiki yangu