RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MATUKIO YA TAMASHA LA FLORA MBASHA SEHEMU YA PILI NDANI YA UBUNGO PLAZA-DAR ES SALAAM

Jina la Flora Mbasha sio geni masikio mwa watu wengi duniani. Flora Mbasha amejulikana kutokana na uimbaji wake wa nyimbo za Injili nchini na nje ya Tanzania. Huduma yake hii imewagusa watu wengi sana na na kusabaisha watu kuweza kuokoka.

Rumafrica ilibahatika kuhudhuria tamasha la Flora Mbasha siku ya Jumapili 14/06/2015 katika ukumbi wa Ubungo Plaza na kuweza kujifunza mengi sana kutoka kwa mkongwe wa nyimbo za Injili Tanzania Flora Mbasha.
Kwanza, kitu nilichojifunza ni KUJIAMINI, Flora Mbasha ikiwa ni mara yake ya kwanza kufanya tamasha katika jiji la Dar es Salaam, aliweza kuthubutu kufanya tamasha lake la LIVE akiwa na bendi yake ambayo ilitambulishwa siku hiyo kwa mara ya kwanza kabisa.

Pili, ni UWEZO wa kutawala jukwaa, Flora alionekana kulimudu jukwaa kama vile ameshawahi kufanya tamasha la LIVE,

Tatu, HISIA, Flora Mbasha aliweza kuimba nyimbo zake za kuabudu kwa hisia sana mpaka ikasababisha watu wote kukaa kimia huku wengine wakitoa machozi, ilifika kipindi hata mgeni Rasmi Mh. Freeman Mbowe kubaki akishangaa jinsi Flora Mbashaalivyokuwa  akiimba kwa hisia, Flora Mbasha aliweza kutoa machozi baada ya kumaliza kuimba wimbo wake wa kuabudu, na hii inaonyesha ni jinsi gani hata yeye  mwenyewe anavyoweza kuguswa na kile anachokiimba.

Nne, KUPENDWA, nasema hivi ni kutokana na jinsi nilivyoshudia watu kutoka Mwanza, Kigoma na Morogoro waliokuja kumuona Flora Mbasha akiimba baada ya kukaa kimia sana kwa muda mrefu. Mwimbaji mmoja anayeitwa Ency Mwalukasa alishudia kuwa yeye binafsi anampenda sana Flora Mbasha, na nyimbo zake huwa zinamgusa sana na kuinua imani yake na Mungu wake.

Sasa tuone matukio haya, na tutazidi kuwaletea matukio mengine, zidi kutembelea blogu yetu hii. Picha zimepigwa na Rumafrica +255 715 851 523

 Ambwene Masongwe akiimba huku wadau wake wakimpongeza kwa fedha
 Dada alitesoma Risala akimtunza Ambwene Mwasongwe


 Elizabeth Ngaiza
  Elizabeth Ngaiza
  Elizabeth Ngaiza
Kutoka kulia ni Christina Mbilinyi, Christopher Mwahangilam (hajajulikana), Furaha Isanya, MC Joyce Ombeni, MC Bony Magupa
 Mwimbaji wa nyimbo za Injili Glory Mainah
 Christina Mbilinyi na Christopher Mwahangila
 Mwimbaji wa nyimbo za Injili Neema Gasper


 Enct Mwalukasa (kulia)
 Rafiki yake Flora Mbasha kutoka USA
 Kutoka kulia ni Glory Mainah, Elizabeth Ngaiza na Sarah Mvungi

 Dancers wa Mch, Maximillian Majeshi Majeshi

 Jesca Sanga (kushoto) na Judith Sanga

 Christopher Mwahangila
 Mama mzazi wa Flora Mbasha
  Christopher Mwahangila
 Mwimbaji wa nyimbo za Injili Neema Gasper akimpongeza Christopher Mwahangila
 Glory Mainah na Elizabeth Ngaiza (kulia)
MC Bony Magupa akimhoji Christopher Mwahangiala


Comments